WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA
MAKAZI
CHUO CHA ARDHI TABORA
ARDHI INSTITUTE TABORA (ARITA)
KATIBA
YA
JUMUIYA YA WANACHUO WA CHUO CHA
ARDHI TABORA
(Ardhi
Institute Tabora Students’ Organization: (ARITASO)
21 Octoba 2013
|
UTANGULIZI
Katiba hii ni
matokeo ya maoni ya wanachuo wa Chuo cha Ardhi Tabora na imeandaliwa na Baraza
la Wawakilishi la ARITASO kwa kuzingatia kifungu cha ibara 8.8 (l) cha katiba
ya ARITASO ya mwaka 2006.
SHUKRANI
Shukrani ziwaendee
wote waliochangia maoni
yao kwa ajiri
ya kukamilisha mchakato mzima wa
Katiba hii ya
JUMUIA YA WANACHUO
CHUO CHA ARDHI
TABORA. Pia Tume inapenda
kuwashukru watu wafuatao;
(i)Mkuu wa chuo
(ii)Mwanasheria mkuu
wa mkoani Tabora.
(iii)Wakufunzi wote
wa chuo.
(iv)Wafanyakazi wote
wa chuo
(v)Serikali
ya wanachuo
(vi)Baraza la wawakilishi
la Aritaso.
(vi)Taasisi
mbalimbali.
(vii)Mlezi wa
wanachuo
(viii)Wanachuo wote.
(ix)Wataalamu
mbalimbali wa masuala ya katiba na watu binafsi.
Imechapishwa:
Matendo E. Kabitagi.
Waziri wa Sheria na
Katiba ARITASO
21
Octoba 2013
MKUU WA
CHUO
………………………….
Tamko
Sisi Wanachuo wa
Chuo cha Ardhi Tabora tunaelewa na kuamini kuwa;
Chuo hiki kina
umuhimu wa pekee katika maendeleo ya nchi yetu.
Na kwamba
Umoja wa
Wanachuo ulio adilifu na wa kidemokrasia ndiyo utakaoweza kusimamia maslahi ya
Wanachuo kikamilifu.
Hivyo basi sisi
Wanachuo wa Chuo cha Ardhi Tabora tunatamka rasmi kuwa;
Kutakuwa na
Umoja wa Wanachuo wa Chuo cha Ardhi Tabora utakaojulikana kwa jina la:
UMOJA
WA WANACHUO WA CHUO CHA ARDHI TABORA
au
ARDHI
INSTITUTE TABORA STUDENTS’ ORGANIZATION (ARITASO)
Ambao utakuwa na Madaraka yote ya
Kikatiba kulingana na kanuni na Sheria za Chuo kama Ifuatavyo:
IBARA
YA KWANZA
JINA, MAKAO MAKUU, KAULI
MBIU, ANUANI NA LUGHA RASMI YA ARITASO
1.1
Jina la umoja wa Wanachuo wa Chuo cha Ardhi Tabora litakuwa:
UMOJA WA WANACHUO CHUO
CHA ARDHI TABORA (ARITASO)
1.2 Makao Makuu ya ARITASO yatakuwa katika Chuo
cha Ardhi Tabora.
1.3 Kauli mbiu ya Chuo ni “TAALUMA BORA YA ARDHI,
MAENDELEO KWA TAIFA”
1.4 Anuani ya Chuo ni:-
CHUO CHA ARDHI TABORA,
S.L.P. 744, TABORA.
SIMU: 026-260-4591.
FAX: 026-260-4928.
Email: arita744@yahoo.co.uk
E-mail ya ARITASO; aritaso@arita.ac.tz
Blogu ya ARITASO: aritasoblog.blogspot.com
Lugha rasmi;
Itakuwa ni Kiswahili
na Kiingereza
IBARA YA PILI
UFAFANUZI
WA MANENO NA VIFUPISHO
Katika katiba hii ila iwapo
maelezo yanayohitaji vinginevyo:-
Chuo cha Ardhi Tabora: Maana yake ni majengo, samani na jumuiya ya watu wote
wanaoishi katika Chuo cha Ardhi Tabora.
2.1 Mwanachuo: Maana yake ni mtu yeyote anayesoma katika Chuo cha Ardhi Tabora.
2.2 Umoja wa wanachuo: Maana yake ni Umoja wa Wanachuo wote wanasoma chuo cha
Ardhi Tabora chini ya ARDHI INSTITUTE TABORA STUDENTS’ ORGANIZATION (ARITASO)
2.3
Chuo: Maana yake
ni Chuo cha Ardhi Tabora.
2.4
Baraza la
Uendeshaji: Maana yake ni Rais, Makamu wa Rais, Katibu
Mkuu, Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara zote za ARITASO.
2.5
Waziri: Maana yake
ni kiongozi wa Wizara yoyote ya ARITASO.
2.6
Viongozi
Wakuu: Maana yake ni viongozi wakuu wa ARITASO
ambao ni:-
i)
Mwenyekiti
ii)
Makamu Mwenyekiti
iii)
Katibu mkuu
2.7 Baraza la Wawakilishi: Maana yake ni Wawakilishi wote wa Wanachuo wa Chuo cha
Ardhi Tabora ambao ni viongozi wote wa Aritaso ,Viongozi wa Mabweni na Wawakilishi
wa madarasa
2.8 Spika: Maana yake kiongozi mkuu wa Baraza la wawakilishi na ndiye
anayepaswa kuongoza vikao vyote vya Baraza la wawakilishi.
2.9 Naibu Spika: Maana yake ni Makamu wa Spika wa Baraza la Wawakilishi.
2.10
Kamati ya Nidhamu:
Maana yake ni kamati ya ARITASO inayoshughulikia nidhamu na maadili ya
wana –ARITASO.
2.11Tume ya Uchaguzi: Maana yake ni kamati maalumu inayoshughulikia masuala
yote ya chaguzi za ARITASO
2.12 Uchaguzi Mkuu: Maana yake uchaguzi wa Rais na Makamu wa Rais.
IBARA
YA TATU
MADHUMUNI;
3. Madhumuni ya ARITASO yatakuwa kama ifuatavyo:-
a)
Kuwa chombo cha pekee cha kulinda maslahi ya Wanachuo kwa muda
wote wanapokuwa Chuoni.
b)
Kujenga moyo wa kuheshimiana kusaidiana na kupendana baina ya
Wanachuo na Jumuiya nyingine.
c)
Kuweka mawasiliano sahihi na ya kindugu baina ya Wanachuo na
Uongozi wa Chuo pamoja na kudumisha uhusiano mzuri kati ya Wanachuo na Walimu /
Wakufunzi, Wafanyakazi na jumuiya yote ya Chuo cha Ardhi Tabora, ili kuhakikisha
Wanachuo wanapatiwa Elimu bora na inayoendana na wakati.
d)
Kuhakikisha kwamba kila Mwanachuo anaelewa na anatekeleza
kikamilifu wajibu wake wa kujielimisha kwa kadiri ya uwezo wake.
e)
Kuimarisha ari ya kusoma na kujenga mazingira bora ya usomaji.
f)
Kuendeleza ari ya kuheshimu Mamlaka na kujielimisha.
g)
Kudumisha na kuendeleza utamaduni wa Taifa letu na kujenga moyo wa
kupenda utamaduni wa taifa letu ili Chuo kiwe mahali pa kuzalisha mabingwa wa
fani mbalimbali.
h)
Kuanzisha na kudumisha uhusiano mwema na Wanachuo wa Vyuo vingine
hapa nchini, Afrika na duniani kote.
i)
Kufanya kila jitihada ya kuhakikisha kuwa madhumuni yaliyoelezwa
hapa yanatekelezwa ipasavyo.
j) Kubuni, kuanzisha,kusimamia
na kuboresha miradi ya kuwasaidia wana Aritaso waliopo na wajao kwa mtindo wa
kupeana kijiti.
IBARA
YA NNE
KAZI
ZA ARITASO:
4.0Majukumu ya ARITASO.
Kwa kushirikiana na Mshauri wa Wanachuo (Dean of Students) katika
kutekeleza madhumuni yake yaliyotajwa katika ibara ya tatu ya katiba hii,
ARITASO itatekeleza kazi zifuatazo.
a)
Kuandaa shughuli mbalimbali kwa ajili ya manufaa ya Wanachuo.
b)
Kuandaa midahalo, semina, warsha, mikutano na ziara za kielimu kwa
kushirikiana na mamlaka ya Chuo ili kubadilishana uzoefu na kupanuana mawazo.
c)
Kuchapisha jarida, vitabu, gazeti n.k, kwa madhumuni ya kupashana
habari.
d)
Kushiriki katika shughuli za kutafuta fedha kadiri umoja wa
Wanachuo utakavyoona inafaa na kukubalika na mamlaka ya Chuo.
e)
Kuwaalika Viongozi
mbalimbali kuja kuzungumza na Wanachuo baada ya kuwasiliana na mamlaka ya Chuo
kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kitamaduni.
f)
Kukuza mawasiliano na kuimarisha uhusiano kati ya jumuiya nyingine
za wanachuo ambazo zina madhumuni yanayolingana na yale ya ARITASO.
g)
Kuanzisha kamati ya Sekretarieti au Tume kwa ajli ya kuboresha
utekelezaji wa madhumuni ya umoja huu.
h)
Kuimarisha shughuli yoyote ambayo inahusiana na madhumuni ya
katiba hii.
i)
Kumfariji kwa hali na
mali mwanachuo yeyote anayepatwa na
matatizo kama
vile
kufiwa, kuugua au kupatwa na ajali.
j)
Kuwawakilisha wanachuo kwenye vyombo vya Chuo vya maamuzi na katika
vyombo
vingine vya maamuzi ndani na nje ya Chuo kadri itakavyohitajika.
k) Kuandaa hatua madhubuti za kushughulikia malalamiko ya wanachuo na
kuyapatia ufumbuzi kwa kushirikiana na Uongozi wa Chuo.
IBARA
YA TANO
KANUNI,
TARATIBU NA MAMLAKA YA ARITASO
5.1 Kanuni na Taratibu za ARITASO
Katika
utendaji kazi wake, ARITASO itatii sheria zote za Jamhuri ya muungano wa
Tanzania. ARITASO itafuata sheria, kanuni na taratibu za Chuo cha Ardhi Tabora.
Pamoja na hayo itaongozwa na kanuni zifuatazo;-
a)Uwazi na ukweli katika
mambo yake yote
b)
Uwajibikaji katika kanuni na matendo yake
c)Kutathmini uwajibikaji wake
ili kuboresha utendaji kazi
d)
Kuzingatia maadili yanayokubalika katika jamii
e)ARITASO itaheshimu na
kuzingatia haki sawa kwa wanachuo wote bila kujali tofauti zao za jinsi, dini,
imani, rangi, kabila, ulemavu, umri, ndoa, taifa au utofauti wa kozi.
5.2 Mamlaka
ARITASO kwa kushirikiana na Mshauri wa
wanachuo (Dean of Students)
Itakuwa
Mamlaka ifuatayo:
a)
Kuandaa katiba ya ARITASO
b)
Kuandaa kanuni na taratibu za Uchaguzi na kuendesha chaguzi zote
za ARITASO
c)
Kuandaa mikakati , sera na miongozo mizuri ya kujenga ARITASO
d)
Kuandaa kanuni na taratibu
nzuri za uendeshaji wa miradi na
matumizi ya fedha ya ARITASO
e)
Kuandaa kanuni na taratibu za utoaji wa huduma kwa wana-ARITASO.
f)
Kushirikiana na kutekeleza mipango mbalimbali hapa chuoni kadri
itakavyoona inafaa.
g)
Kumchukulia hatua za kinidhamu mwanachuo yeyote atakaye vunja
sheria, kanuni na taratibu za Chuo au/na katiba ya ARITASO kupitia Kamati yake
ya Nidhamu kwa mujibu wa kanuni na sheria za Chuo.
IBARA
YA SITA
UANACHAMA:
6.1 Kujiunga na Muungano wa wanachuo;-
Mtu yeyote ambaye amesajiliwa kusoma
katika Chuo cha Ardhi Tabora
atakuwa Mwanachama wa ARITASO moja kwa moja hadi atakapomaliza mafunzo yake
endapo hatafukuzwa Chuo au kusitishiwa
masomo yake.
6.2 Vigezo na Masharti
ya uanachama wa ARITASO
a)
Mwanachama wa ARITASO atatakiwa kulipa ada ya uanachama kiasi cha
Tsh. 10,000/= kwa mwaka mara afikapo hapa Chuoni. Kiwango hiki kinaweza
kubadilika kulingana na kupanda kwa gharama za maisha, pia hakirudishwi. Baraza
la wawakilishi litapitisha mabadiliko hayo.
b)
Mwanachama atafaidika au kunufaika na mradi wa Aritaso pale
atakapotoa matunda mazuri na pia kuchangia uboreshwaji wa miradi utakapopata
hasara au kuhujumiwa.
c)
Mwanachama anatakiwa kuwa mwajibikaji katika shughuli zote za
ARITASO.
6.3 Kusitishwa uanachama.
Mwanachama wa ARITASO atahesabiwa kwamba
sio mwanachama wa ARITASO
endapo hatakuwa mwanachuo wa Chuo cha
Ardhi Tabora kwa sababu yoyote ile.
IBARA
YA SABA
HAKI
ZA MWANACHAMA
7.1 Mwanachama wa ARITASO atakuwa na Haki zifuatazo:-
a.
Kushiriki katika shughuli zote zinazoandaliwa na ARITASO pamoja na
mamlaka ya Chuo.
b.
Kuchagua, kuchaguliwa, au
kuteuliwa katika nafasi yoyote ya Uongozi wa ARITASO.
c.
Kuangalia/kuona nyaraka za fedha na nyaraka zingine za ARITASO ambazo
ni za bayana baada ya kuomba idhini ya kufanya hivyo kutoka kwa Katibu Mkuu wa
ARITASO.
d.
Kujitetea na kutoa maelezo
yake mbele ya kikao chochote cha ARITASO pamoja na kukata rufaa katika vikao
vya juu yake na kwa kushirikiana na mamlaka ya Chuo.
e.
Kukosoa, pia kukosolewa katika vikao mbalimbali vya ARITASO.
f.
Kutoa mchango wa maoni yake waziwazi na bila woga katika vikao na
mikutano inayomhusu kwa manufaa ya ARITASO na jumuiya nzima ya Chuo cha Ardhi
Tabora.
g.
Kupatiwa matibabu kikamilifu kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na
mamlaka ya Chuo.
IBARA
YA NANE
WAJIBU
WA MWANACHAMA
8.1 Mwanachama wa
ARITASO atakuwa na wajibu ufuatao;-
i)
Kuilinda na kuitii Katiba hii ya ARITASO.
ii)
Kujielimisha na kujiendeleza kwa kadiri ya uwezo wake na kutumia
Elimu yake kwa faida ya Taifa. Kulipa michango mbalimbali ya kikatiba au michango
mingineyo Kama itakavyoamuliwa na ARITASO kwa nyakati mbalinbali.
iii) Kuhudhuria kikamilifu
vipindi vya masomo, mikutano, maandamano halali, na kukamilisha shughuli zote za
kitaaluma anazowajibika nazo kwa wakati kila siku. Kama
vile taaluma, michezo na usafi ambapo ni kwa maeneo husika tu. Kwa mfano;-
madarasani, mabwenini na maeneo yote yanayozunguka madarasa na mabweni.
iv) Kutekeleza misingi ya nidhamu, kushiriki vema katika shughuli za Chuo.
v)
Kutunza, kuthamini na kulinda mali ya
Chuo na miradi yote ya chuo.
vi) Kuendeleza tabia na moyo wa umoja na upendo kwa Wanachuo wenzake na kwa
wanajumuiya wote wa Chuo cha Ardhi Tabora.
vii) Kudumisha nidhamu bora na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kumletea aibu
yeye mwenyewe, ARITASO au Chuo na Taifa kwa ujumla
IBARA YA TISA
VIKAO
VYA ARITASO:
9.1 Vikao halali vya ARITASO vitakuwa kama ifuatavyo:-
a) Mkutano wa Baraza la Uendeshaji.
b)
Vikao vya Kamati ya Nidhamu.
c)
Mkutano mkuu wa Wanachuo wote.
d) Mkutano wa Baraza la Wawakilishi,
e)
Mkutano wa Wanachuo wote na Uongozi wa Chuo.
9.2 Mkutano wa Baraza
la Uendeshaji
a)
Mkutano wa Baraza la Uendeshaji utajumuisha wajumbe wote wa Baraza
hilo na wajumbe wengine ambao litaona vema kuwaalika.
b)
Mkutano wa Baraza la Uendeshaji utakutana si chini ya mara mbili
kwa kila muhula wa masomo.
9.3 Waziri Mkuu atatoa taarifa ya mkutano wa Baraza la
Uendeshaji
a)
Baada ya kuombwa na Rais kufanya hivyo au
b)
Baada ya kupokea ombi la maandishi lililotiwa sahihi na theluthi
moja ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi au robo ya Wanachuo wote.
c)
Katibu Mkuu atatoa taarifa ya Mkutano wa Baraza la Uendeshaji ndani
ya siku tatu baada ya kutakiwa kufanya hivyo.
9.1
Rais wa ARITASO atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa
Serikali ya Wanachuo, kama hayupo Makamu wa Rais
ataongoza Mkutano.
9.2
Kiwango cha wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Uendeshaji
Mkutano wa Baraza la Uendeshaji utatakiwa
uwe na zaidi ya nusu ya wajumbe wote
wanaostahili kuhudhuria mkutano huo.
9.4 Kazi za Mkutano wa Baraza la Uendeshaji:-
- Kuzungumzia
mambo yote yanayohusu maslahi ya Wanachuo.
- Kujadili na kutoa maamuzi juu ya mapendekezo yoyote
ya vikao vya chini yake ikiwa ni pamoja na kukubali au kutokubali hoja
kutoka Baraza la Wawakilishi ya kutokuwa na imani na Rais wa ARITASO bila
kuathiri kipengele cha (11.2.0) cha katiba hii.
- Kupitisha
taarifa mbalimbali zitakazotolewa na Baraza la Wawakilishi.
- Kujadili na
kupitisha Katiba ya ARITASO itakayoandaliwa na Baraza la Wawakilishi.
9.5 Mkutano Mkuu wa Wanachuo wote:-
a. Mkutano mkuu wa Wanachuo wote utajumuisha Wanachuo wote wanaochukua mafunzo
katika Chuo cha Ardhi Tabora.
b. Mkutano mkuu wa Wanachuo wote utakutana si chini ya mara moja kwa muhula,
ila Mkutano Maalum unaweza kuitishwa wakati wowote ili kujadili masuala muhimu
ya dharura.
c. Rais wa ARITASO ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano mkuu wa Wanachuo wote,
kama hayupo Makamu wa Rais ataongoza mkutano.
d. Kiwango cha wajumbe wa Mkutano mkuu wa Wanachuo wote kitakuwa zaidi ya nusu
ya wajumbe wote wanaostahili kuhudhuria Mkutano wa Wanachuo wote ama Mkutano
maalum.
e. Mkuu wa Chuo
atakutana na Wanachuo mara mbili kwa
muhula au zaidi pale itakapoonekana kuna haja ya Wanachuo kuonana naye.
9.6 Kazi za Mkutano mkuu wa Wanachuo wote.
a. Kuchambua
na kuzitolea maamuzi au ushauri taarifa zinazowasilishwa kwake na Baraza la Uendeshaji.
b. Kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi na maendeleo kwa Wanachuo na Chuo
kwa ujumla
c. Utawachagua Rais na Makamu wa Rais wa ARITASO inapofikia wakati wa
uchaguzi.
IBARA
YA KUMI
MIHIMILI YA
ARITASO
10.1 Kutakuwa
na Mihimili mikuu mitatu ya ARITASO, ambayo ni;
i)
Baraza la Uendeshaji (Serikali ya ARITASO
inayochaguliwa na wanachuo)
ii) Baraza la Wawakilishi
iii) Kamati ya Nidhamu
Kila Mhimili utajitegemea
katika utendaji kazi wake.
10.2 BARAZA LA
WAWAKILISHI
Kutakuwa
na Baraza la Wawakilishi la ARITASO ambalo litakuwa na
Wajumbe wafuatao:-
a.
Spika wa Baraza la Wawakilishi
b.
Naibu Spika
c.
Katibu Mkuu wa Baraza la Wawakilishi
d.
Baraza la Uendeshaji
e.
Wenyeviti wa Mabweni
f.
Makatibu wa Mabweni
g.
Mwakilishi mmoja toka kila darasa
10.3 Mikutano ya
Baraza la Wawakilishi.
a) Baraza la Wawakilishi litakutana si chini ya mara tatu kwa muhula.
b) Spika ataongoza mikutano yote ya Baraza la Wawakilishi, kama hayupo Naibu
Spika atashika nafasi hiyo, na kama wote wawili hawapo kikao kitamchagua Mwenyekiti
wa muda.
c) Spika atatakiwa kutoa tangazo la kikao hicho kwa umma na barua ya mwaliko
kwa wajumbe wote wa kikao hicho cha Baraza la wawakilishi siku mbili kabla.
Akishindwa kufanya hivyo moja kwa moja atatakiwa kujiudhuru kwenye nafasi yake
na Naibu spika atashikilia nafasi yake.
d) Endapo kuna jambo la dharura, Spika atakuwa na uwezo wa kuitisha kikao cha
dharura cha baraza la wawakilishi endapo tu asilimia ishirini na tano (25%) ya
wajumbe wa kikao hicho wamesaini kukubali kuitishwa kwa kikao hicho. Tangazo la
muda mfupi zaidi(chini ya siku mbili) atalitoa bila kufungwa na kipengele cha 10.3
(c)
10.4
Muda wa uongozi.
a.
Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi wataongoza katika nafasi zao
kwa muda wa mwaka mmoja. Wanaweza kuendelea katika awamu nyingine ya uongozi endapo
watachaguliwa au kuteuliwa tena.
b.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi atasitishwa uanachama wake kwenye Baraza
hilo, ikiwa atabainika na yafuatayo;
i) Kutohudhuria vikao
viwili vya Baraza la wawakilishi bila taarifa yoyote ya Maandishi kwa Spika.
ii) Kifo, kusitisha masomo, kufukuzwa Chuo au
kusitishiwa usajili wa Chuo.
iii)
Mjumbe yeyote wa Baraza la wawakilishi aliyechaguliwa na wanachuo katika
eneo lake mfano kozi yake, bweni lake n.k atasitishwa kuwa mjumbe wa Baraza la wawakilishi endapo Spika atapokea waraka
kutoka kwenye eneo hilo uliosainiwa na
wajumbe wasiopungua theruthi mbili ya watu
wote wanaokaa eneo hilo unaotaka aondolewe kwenye nafasi
yake ya kuwa mjumbe wa Baraza la
wawakilishi.
iv)
Kuondolewa katika nafasi yake anayoiwakilisha kwenye Baraza la Wawakilishi kutoka kwenye eneo analoliwakilisha.
10.5 Malipo ya wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi.
a.
Wajumbe wote wa Baraza la wawakilishi hawatalipwa mshahara wowote isipokuwa
tu watawezeshwa kifedha ili
kufanikisha kutekeleza majukumu yao.
b.
Asilimia ishirini (20%) ya mapato yote ya mwaka ya ARITASO itatumika
Kuwawezesha kifedha viongozi katika utaratibu
ufuatao:-
i) Baraza
la Uendeshaji - Asilimia arobaini na tano (45%) ya hiyo asilimia ishirini
ii) Baraza la Wawakilishi –
Asilimia ishirini na tano (25%) ya hiyo asilimia ishirini
iii)
Kamati ya nidhamu – Asilimia tisa (9%) ya hiyo asilimia ishirini
iv)
Tume ya Uchaguzi – Asilimia ishirini na moja (21%) ya hiyo
asilimia ishirini
NB: Uwezeshwaji huu utafanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za
ARITASO kwa kushirikiana na Mshauri wa wanachuo na kiwango hicho kinaweza
kubadilika kutokana na sababu mbalimbali.
Baraza la Wawakilishi litahusika kufanya mabadiliko hayo kama litakavyoona
inafaa.
10.6 Kazi za Baraza la
Wawakilishi
Baraza la Wawakilishi litakuwa na kazi
zifuatazo:-
a.
Kumchagua Spika, Naibu Spika na Katibu wa Baraza la wawakilishi.
b.
Kuthibitisha Mawaziri na Makatibu waliopendekezwa na Mwenyekiti kwa
kushirikiana na Makamu wa Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa ARITASO.
c.
Kuthibitisha Majina ya Wajumbe wasiopungua watano wa kuingia
katika kila Wizara kama yatakavyopendekezwa na kamati ya Uendeshaji.
d.
Kuziangalia na kuzikubali au kuzikataa sera na mwenendo wa Baraza
la Uendeshaji.
e.
Kupitisha makisio ya mapato na matumizi ya ARITASO kama
yatakavyowasilishwa na Katibu Mkuu baada ya kutayarishwa na kamati ya
Uendeshaji.
f.
Kuweka utaratibu wa uendeshaji wa mambo yote yanayohusu fedha za
miradi ya ARITASO, ukaguzi wa mara kwa mara wa vitabu vya mahesabu na kutoa
ripoti ya mwaka ya ukaguzi wa mahesabu yote.
g.
Kumteua mkaguzi wa ndani wa mahesabu ya ARITASO.
h.
Kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za kinidhamu au za kisheria
dhidi ya kiongozi yeyote wa ARITASO ama wengineo atakayebainika kuwa amehusika
na matumizi mabaya ya fedha za ARITASO au ubadhirifu wa aina yoyote.
i.
Kumwondoa
Madarakani Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa ARITASO kwa kutumia utaratibu ulioainishwa kwenye ibara
11.2.0 ya katiba hii.
j.
Kuunda Idara na kamati za ARITASO kama zitakavyowasilishwa na
kamati ya Uendeshaji kadiri itakavyoonekana ni lazima kwa ajili ya utekelezaji
wa shughuli mbalimbali.
k.
Kupokea Taarifa za Wizara na kamati za ARITASO.
l.
Kuandaa rasimu ya katiba ya ARITASO na kuipeleka mbele ya Mkutano
Mkuu wa Wanachuo kwa kujadiliwa na kuthibitishwa kama ilivyoanishwa katika
ibara ya 13. Ya katiba hii.
m.
Kufanya kazi zozote kama Mkutano Mkuu wa Serikali ya Wanachuo au/na
Mkutano wa Wanachuo wote utakavyoagiza.
10.7 Spika wa Baraza la wawakilishi.
i) Kutakuwa na Spika wa Baraza la wawakilishi atakaye
chaguliwa kutoka miongoni wa wajumbe wa baraza hilo.
ii) Spika hatakuwa mjumbe wa Baraza la Uendeshaji
la ARITASO.
i)
Spika ataongoza vikao vyote vya Baraza la wawakilishi kwa mujibu
wa kanuni na taratibu zote za Baraza hilo lililojiwekea.
ii)
Endapo Spika atavunja
kipengele chochote cha katiba hii, Baraza
la
Wawakilishi litakuwa na uwezo wa kumwondoa
katika nafasi yake ya uspika kwa
Wajumbe wa Baraza hili kupiga kura
zisizopungua theluthi mbili ya wajumbe
wote wa baraza hili.
v)
Spika atakuwa mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi popote
itakapohitajika uwakilishi wa Baraza
hili.
10.8 Naibu Spika
i)
Kutakuwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi atakaye chaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe wa baraza hili.
ii)
Naibu Spika hatakuwa mjumbe wa Baraza la Uendeshaji la ARITASO. Na
atatakiwa kuongoza vikao vyote vya Baraza la Wawakilishi endapo Spika hayupo.
iii)
Naibu Spika ataondolewa madarakani vilevile kama atakavyoondolewa
Spika kama ilivyotamkwa kwanye ibara ya 10.7. (iv) ya katiba hii.
10.9 Katibu wa Baraza
la Wawakilishi.
i)
Kutakuwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi ambaye atachaguliwa na
wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka
miongoni mwa wanachama wa ARITASO.
ii)
Katibu wa Baraza la Wawakilishi
atakuwa ndiye mwandishi na mtunza nyaraka
zote za Baraza la Wawakilishi. Pia atalazimika kufuata kanuni na taratibu zote za baraza hili lillojiwekea.
iii)
Katibu wa Baraza la Wawakilishi anaweza kuondolewa madarakani kama
Anavyoodolewa Spika wa Baraza
hili kama ilivyotamkwa kwanye ibara ya 10.7.(iv) ya katiba hii.
10.10 BARAZA LA UENDESHAJI
i)
Kutakuwa na Baraza la Uendeshaji la ARITASO ambalo litakuwa ndicho
chombo cha kusimamia utekelezaji wa
shughuli za kila siku za ARITASO. Baraza hili litakuwa na Wajumbe wafuatao:-
a)
Rais wa ARITASO
b)
Makamu wa Rais wa ARITASO
c)
Katibu Mkuu wa ARITASO
d)
Mawaziri wote wa Wizara za ARITASO
e)
Manaibu Mawaziri wote wa Wizara zote za ARITASO.
ii) Baraza la
Uendeshaji litakutana si chini ya mara tatu kila muhula.
iii)
Baraza la Uendeshaji litakuwa na wajumbe wasiozidi ishirini na moja ambao watateuliwa kutoka miongoni mwa wanachama wa ARITASO.
iv)
Baraza la Uendeshaji litakuwa ndicho
chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo
yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya
Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri
Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa
maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.
v)
Rais wa ARITASO ataongoza vikao vyote vya Baraza la Uendeshaji.
vi)
Makamu wa Rais wa ARITASO atakaimu nafasi ya Rais kama Rais
hayupo.
vii)
Mwenyekiti wa muda atateuliwa kuendesha kikao kama Rais na Makamu
wa Rais hawapo.
10.11 Muda wa Uongozi.
a)
Mawaziri wote, manaibu waziri wote na makatibu wote wa wizara zote
za ARITASO wataongoza katika nafasi zao kwa muda wa mwaka mmoja. Wanaweza
kuendelea katika awamu nyingine ya uongozi endapo watachaguliwa au kuteuliwa
tena.
b)
Waziri yeyote, naibu waziri yeyote au katibu yeyote wa wizara yoyote ya ARITASO atavuliwa nafasi yake ya
uwaziri au unaibu waziri au ukatibu kwenye Baraza hilo, endapo atabainika na
yafuatayo;
i) Kutohudhuria vikao
viwili vya Baraza la Uendeshaji bila taarifa yoyote ya maandishi kwa katibu mkuu wa ARITASO
ii ) Kifo, kusitisha
masomo, kufukuzwa Chuo au kusitishiwa usajili wa Chuo.
iii) Rais wa ARITASO atakuwa na mamlaka ya kumwondoa Madarakani Waziri
yeyote au naibu waziri yeyote kwa barua kwa utovu wa nidhamu au kwa kushindwa kutekeleza majukumu
yake na atateua mtu Mwingine kushikilia
nafasi yake. Rais wa ARITASO atatoa taarifa
kwa barua kwenye Baraza la Wawakilishi juu ya uamuzi aliouchukua wa kumwondoa madarakani kiongozi huyo.
10.12 Kazi za Baraza
la Uendeshaji:-
a. Kuongoza na kuendesha shughuli za kila siku za Wanachuo kwa mujibu wa
Katiba hii na kama itakavyoagizwa na vikao vya juu vya ARITASO.
b.
Kusimamia maslahi ya kila siku ya Wanachuo.
c.
Kuidhinisha na kuthibitisha mapato na matumizi yote ya fedha za
miradi ya Wanachuo.
d.
Kusimamia uzalishajimali na shughuli za uchumi za Wanachuo.
e.
Kusimamia utekelezaji wa Kanuni za Chuo na nidhamu ya Wanachuo kwa
ujumla.
f.
Kupendekeza Wizara na kamati mbalimbali za ARITASO na kuwasilisha
mbele ya
Baraza la Wawakilishi kwa uthibitisho, kwa mfano:-
i. Wizara ya Chakula
(Cafeteria)
ii. Wizara ya Afya na Mazingira
iii. Wizara ya Michezo, Habari na Mawasiliano
iv. Wizara ya Elimu
v. Wizara ya Sheria na Katiba
vi. Wizara ya Mambo ya Ndani
vii. Wizara ya Ulinzi na Usalama
viii. Wizara ya Mambo ya Nje na
Uhusiano.
g.
Kuandaa
makisio ya mapato na matumizi ya ARITASO
ya kila Wizara yatakavyowasilishwa na Waziri husika wa kila Wizara
kwenye Baraza la wawakilishi.
h.
Kuandaa miswaada, kanuni, taratibu na sheria za ARITASO
zitakazowasilishwa kwenye Baraza la wawakilishi ili kuidhinishwa.
i.
Ili kuondoa wasiwasi Mawaziri wote, manaibu waziri wote na makatibu wa Wizara
zote, wote watawajibika kwa Rais
wa ARITASO.
10.13 Malipo ya wajumbe wa Baraza la Uendeshaji
Ili kuondoa wasiwasi Wajumbe wote wa Baraza la wawakilishi
hawatalipwa mshahara
wowote isipokuwa watawezeshwa
kifedha ili kufanikisha utendaji kazi wao kama ilivyo tamkwa katika ibara ya
10.5 (b) ya katiba hii.
10.14 KAMATI YA NIDHAMU
a)
Kutakuwa na Kamati ya nidhamu ya ARITASO ambayo itateuliwa na
Raisi wa Aritaso mara baada ya kuingia madarakani. Kamati hii itakuwa na Mwenyekiti
na Katibu ambao ni waziri wa sheria na
katiba pamoja na katibu kutoka ndani ya wajumbe wa kamati hiyo..
b)
Wajumbe wa kamati hii ni;-
i)
Mwenyekiti wa kamati
ii)
Katibu wa kamati
iii)
Mjumbe mmoja mmoja toka
kila darasa.
10.15 Kazi za Kamati ya Nidhamu
i)
Ni chombo cha kudhibiti nidhamu ya wanachama wa ARITASO. Kamati hii
itakuwa ndicho chombo chenye mamlaka ya
kutoa adhabu kwa ngazi ya wanachuo na kitatoa adhabu kwa mwanachuo yeyote isipokuwa kwa Rais na Makamu
wa Rais. Kamati hii itatoa adhabu kwa makosa ya ubadhilifu wa mali ya ARITASO,
rushwa na makosa mengine yote ya utovu wa nidhamu.
ii) Kuandaa kanuni na taratibu zote kwa ajili ya kupokea na
kutatua migogoro miongoni mwa wanachuo
ili kuondoa matabaka ya ukozi rangi, jinsia n.k na ili kuleta
haki, usawa, umoja na mshikamano miongoni mwa wanachuo.
iii) Kutekeleza maelekezo au majukumu yatakayotolewa na Baraza la wawakilishi,
Baraza la Uendeshaji au mwana ARITASO
yeyote kama kuna hitajika kufanya hivyo.
10.16 Mipaka ya utendaji wa kazi yake
a)
Kwa kushirikiana na mshauri wa wanachuo, kamati ya nidhamu ya
Aritaso itakuwa ndicho chombo cha mwisho katika kutoa maamuzi ya migogoro
chuoni ngazi ya wanachuo na yale yote yatakayoshindikana kupatiwa ufumbuzi
katika kamati hii, kwa maandishi itayawasilisha kwenye ngazi ya Chuo ili
kupatiwa ufumbuzi.
b)
Endapo kutahitajika, kamati hii inaweza kumwalika Rais wa ARITASO,
Makamu wa Rais, Spika, kiongozi yeyote
au mtu yeyote ambaye kwa namna moja au nyingine kamati itamwitaji ili
atoe mawazo yake, ushauri au/na ushahidi wa mambo mbalimbali yanayo hitaji
msaada wake.
10.17 Muda wa uongozi
a)
Kamati hii itaongoza kwa muda wa mwaka mmoja tangu iingie
madarakani.
b)
Mjumbe yeyote wa kamati hii atatakiwa kuondoka madarakani mara
moja iwapo asipohudhuria vikao viwili vya kamati hii bila taarifa yoyote ya
maandishi kwa Mwenyekiti wa kamati au kwa mtu yeyote anayekaimu nafasi hiyo.
10.18 Vikao vya Kamati ya Nidhamu
a)
Vikao vyote vya Kamati ya nidhamu vitaandaliwa na katibu wa kamati
hii baada ya kushauriana na mwenyekiti wa kamati hii. Katibu atatakiwa kutoa
tangazo la kikao hiki siku moja kabla ya siku ya kikao hicho.
b)
Wajumbe katika kikao hiki wanatakiwa wasipungue theluthi mbili ya
wajumbe wote.
c)
Baraza hili litafanya vikao visivyopungua vitatu kila muhula
wa masomo.
d)
Endapo katibu wa Kamati hii atashindwa kuitisha kikao cha
Kamati au likitokea swala linalohitaji
ulazima wa kuitisha kikao cha kamati, theluthi moja ya wajumbe wa kamati hii
watakubaliana watamwomba katibu wa kamati
kuitisha kikao cha kamati hii ili kutatua swala lililojitokeza.
10.19 Malipo ya wajumbe wa Kamati ya Nidhamu
Ili kuondoa wasiwasi, Wajumbe
wote wa Kamati ya Nidhamu hawatalipwa mshahara isipokuwa watawezeshwa kidogo
kifedha ili kufanikisha utendaji kazi wao kama ilivyo tamkwa katika ibara ya
10.5 (b) ya katiba hii.
IBARA YA KUMI NA
MOJA
UONGOZI WA ARITASO NA KAZI ZAO.
11.1 Viongozi wa ARITASO watakuwa:-
a.
Rais i wa ARITASO
b.
Makamu wa Rais wa ARITASO
c.
Katibu Mkuu wa ARITASO
d.
Spika wa Baraza la wawakilishi
e.
Mawaziri wa Wizara zote za ARITASO
f.
Makatibu (ma-Naibu waziri) wa Wizara zote za ARITASO
g.
Wenyeviti wa Mabweni
h.
Makatibu wa Mabweni
i.
Wawakilishi wa Madarasa
j.
Wawakilishi Wasaidizi wa Madarasa
11.2 Rais wa
ARITASO
a)
Rais wa ARITASO atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Wanachuo kwa kura
za siri kwa mujibu wa katiba hii na kwa mujibu wa mwongozo na kanuni zitakazo
kubaliwa na Baraza la wawakilishi.
b)
Rais wa ARITASO ndiye kiongozi Mkuu na Msemaji Mkuu wa ARITASO.
c)
Rais wa ARITASO atakuwa na uwezo wa kuteua Mawaziri wa Wizara
mbalimbali kwa kushirikiana na Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa ARITASO.
d)
Uongozi wa ARITASO utasimikwa rasmi na Uongozi wa Chuo kama
ilivyotamkwa kwenye ibara ya 12. Ya
katiba hii.
e)
Rais wa ARITASO ataongoza vikao vyote vya juu vya ARITASO, Wajumbe
watamchagua Mwenyekiti wa muda iwapo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hawapo
kama kifungu cha Katiba kinavyoagiza.
f)
Ikitokea Ofisi ya Rais wa ARITASO ikabaki wazi kabla ya nusu mwaka
kuisha (nusu ya muda wake wa uongozi), uchaguzi utafanyika haraka ili kuziba
pengo hilo au namna nyingine inaweza kufanyika kama itakavyoamuliwa na Baraza
la wawakilishi ili kuziba pengo hilo na izingatiwe kwamba kama mwenyekiti
amekaa madarakani kwa muda wa nusu mwaka (nusu ya muda wake wa uongozi)
uchaguzi hautafanyika na badala yake makamu mwenyekiti atashikilia ofisi ya Mwenyekiti
wa ARITASO ili kumalizia muda uliobaki.
g)
Sababu za kubaki wazi kwa Ofisi
ya Rais wa ARITASO ;-
i) Kujiuzuru kwa kwa Rais
wa ARITASO
ii)
Kifo
iii)
Kuondolewa madarakani.
iv)
Kusitishiwa masomo au kufukuzwa Chuo
v)
Sababu nyingine yoyote ile inayoweza kupelekea Ofisi ya Rais ARITASO
kubaki wazi.
a)
Endapo Rais wa ARITASO hatakuwepo ofisini kwa sababu yoyote ile kama vile kusafiri au
dharura yoyoye ile, majukumu ya Ofisi ya Rais ARITASO atamwachia yeyote kati ya
hawa wafuatao kwa kufuata mpangilio;
i) Makamu wa Rais ARITASO
ii)
Waziri Mkuu
ii)
Spika
NB.Mtu yeyote kati ya hao
yaani kipengele 11.1.8 a),b),c) hapo juu aliye achiwa madaraka, atakabidhi madaraka
hayo haraka iwezekanavyo, baada ya mtu aliyemkabidhi kurudi.
11.3 Kuvunjika kwa
Serikali
Kama nafasi ya Rais
wa ARITASO na Makamu wa Rais imebaki wazi kwa sababu zozote zile kama katiba
hii inavyotamka, Serikali nzima ya ARITASO itahesabika kuwa imevunjika. Katika
hali hii Wajumbe wengine wa Baraza la Uendeshaji wataendelea kushikilia nafasi
zao za uongozi hadi pale Uchaguzi Mkuu utakapo fanyika ili kumpata Rais na
makamu wa Rais mpya. Uchaguzi huo utatakiwa ufanyike ndani ya siku kumi na nne
baada ya nafasi hizo kubaki wazi.
11.4 Vigezo vitakavyo
tumika kumchagua Rais wa ARITASO.
a)
Mwanachama yeyote wa ARITASO ataruhusiwa kuchaguliwa kuwa Rais wa
ARITASO ikiwa tu ana muda wa mwaka mmoja au zaidi wa uanachama wake ndani ya
ARITASO.
b)
Mtu yeyote anayeshikilia wadhifa wa Rais wa ARITASO ataruhusiwa kugombea
tena katika nafasi hiyo.
c)
Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais wa ARITASO, asipo jiuzuru,au
asipofariki au asipoondolewa madarakani au asipositishiwa masomo yake
atashikilia Ofisi hiyo ya Rais wa ARITASO kwa muda usiopungua mwaka mmoja.
11.5 Kumwondoa Rais wa
ARITASO Madarakani
a)
Baraza
la wawakilishi litakuwa na uwezo wa kupitisha maamuzi ya kumwondoa
Rais wa ARITASO
madarakani kama ilivyotamkwa katika kipengele cha 10.6.(i) cha katiba hii.
b)
Sababu za kumwondoa Rais madarakani ni kama ifuatavyo;-
i)
Akifanya vitendo viovu vinavyovunja katiba hii.
ii)
Akifanya vitendo vinavyoishushia heshima ofisi ya Rais wa ARITASO.
c) Waraka
wowote wa kumwondoa Rais madarakani lazima usainiwe na theluthi
mbili ya wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi
na uambatanishwe na saini za wanachuo
kumi kutoka kila kozi na ziwasilishwe kwa Spika.
d)
Kabla ya Baraza
la Wawakilishi kutoa maamuzi ya kumwondoa Rais madarakani, yafuatayo yatazingatiwa;-
i)
Kwa
idhini ya maadishi ya Spika, itaundwa kamati ya uchunguzi ya watu watano, na
majina yao yataidhinishwa na theluthi mbili ya wajumbe wote Baraza la Wawakilishi.
ii)
Kamati
hii itafanya uchunguzi juu ya tuhuma kwa Rais na itatakiwa itoe taarifa yake ya
uchunguzi kwa Spika ndani ya siku saba
toka siku majina ya tume hiyo yalipotangazwa.
iii)
Spika
atatakiwa kumtaarifu Rais juu ya tuhuma zinazomwandama.iv) Spika atakapopokea
ripoti ya kamati ya uchunguzi, atatakiwa kuitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Wawalishi ili ripoti ya
kamati ya uchunguzi isomwe na mwenyekiti wa kamati hiyo mbele ya Baraza la
wawakilishi. Kisha Baraza la wawakilishi litatathmini ripoti hiyo.
iv)
iv)
Spika atampa barua Rais juu ya matokeo ya uchunguzi wa kamati ya uchunguzi pamoja na maamuzi ya Baraza
la wawalishi. Rais atatakiwa kujitetea
juu ya tuhuma hizo na atatakiwa
kutoa taarifa yake ya kujitetea ndani ya siku tatu mbele ya Baraza la
wawakilishi na/au atawasilisha taarifa yake
ya maandishi ya kujitetea kwa Spika.
v)
Spika
atatakiwa kuitisha Mkutano Maalum wa
Baraza la wawakilishi kwa ajili ya kutoa
maamuzi ya kumwondoa au kutomwondoa Rais madarakani kwa kuzingatia ile ripoti ya
kamati ya uchunguzi na taarifa ya kujitetea ya Rais.Uamuzi wa kumwondoa Rais madarakani
utafikiwa tu endapo theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi
watakubali uamuzi huo.
vi)
Wajumbe
wa Mkutano Maalum wa Baraza la
wawakilishi wa kutoa uamuzi wa kumwondoa au kutomwondoa Rais madarakani
wanatakiwa wasipungue asilimia tisini (90%) ya wajumbe wote wa baraza hilo.
vii) Baraza la wawakilishi litakapopitisha uamuzi
wa kumwondoa Rais madarakani kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na katiba hii,
Rais atatakiwa kuondoka madarakani mara moja mara tu baada ya uamuzi huo
kupitishwa na Baraza hilo na kwamba Serikali yote ya ARITASO itakuwa imevunjika.
Makamu wa Rais na waziri mkuu wataendelea kubaki
madarakani ilimradi wawe hawahusiki na tuhuma za Rais. Na utaratibu wa
kipengele cha 11.2 (f) cha katiba hii utazingatiwa.
11.6 Makamu wa Rais wa
ARITASO
a) Makamu wa Rais wa ARITASO
atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Wanachuo
kwa kura za siri
kwa mujibu wa taratibu zitakazo wekwa na Baraza la
wawakilishi.
b) Makamu wa Rais wa
ARITASO ni msaidizi mkuu wa Rais wa ARITASO.
c) Atakuwa ndiye Mwenyekiti
wa mikutano yote iwapo Rais wa ARITASO hatakuwepo.
d) Atafanya kazi nyingine
zote kwa kushauriana na Rais wa ARITASO.
11.7Katibu Mkuu wa ARITASO.
i) Rais wa ARITASO kwa kushirikiana na Makamu Rais wa ARITASO
watamteua Katibu Mkuu wa ARITASO.
ii) Katibu Mkuu atakuwa ndiye mtendaji mkuu wa ARITASO.
iii) Atashughulikia maswala yote yanayohusu matatizo mbalimbali ya
Wanachuo.
iv) Atakuwa mratibu wa shughuli zote za Wizara na za Kamati
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuandaa taarifa zote za ARITASO.
v) Atakuwa mwandishi wa mihutasari yote ya mikutano yote ya
ARITASO. Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika
kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
11.8 Mawaziri wa Wizara
mbalimbali.
b)
Kutakuwa na Mawaziri mbalimbali wa ARITASO ambao watateuliwa na Rais
kwa kushirikiana na Makamu wa Rais na
Katibu Mkuu wa ARITASO ambao watasimikwa na Uongozi wa Chuo kama ilivyotamkwa
katika ibara ya 13. Ya katiba hii.
iii)
Mawaziri watakuwa ndio watendaji wakuu wa Wizara zao.
Mawaziri
watafanya kazi zote chini ya Uongozi wa Rais, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu.
11.9 Makatibu wa Wizara
i) Kutakuwa na Makatibu wa Wizara mbalimbali za ARITASO ambao ndio
watakaokuwa Ma-Naibu Mawaziri wa Wizara husika.
iv)
Makatibu watasimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku za
Wizara zao.
11.10 Wenyekiti wa
Mabweni
a)
Kutakuwa na Wenyeviti wa Mabweni ya Wanachuo ambao watachaguliwa
na wakazi wote wa Mabweni husika kwa kura za siri.
b)
Mwenyekiti wa bweni atakuwa ndiye Kiongozi Mkuu wa Bweni.
c)
Atakuwa ndiye Mwenyekiti wa vikao vyote vya bweni.
11.11 Makatibu wa mabweni
a)
Kutakuwa na ma-Katibu wa mabweni (ambao ndio Makamu wenyeviti)
katika kila bweni ambao watachaguliwa na Wakazi wote wa bweni linalohusika kwa
kura za siri.
b)
Katibu wa Bweni atakuwa ndiye mtendaji Mkuu wa Bweni.
c)
Katibu wa bweni atafanya kazi zake zote chini ya Baraza la Uendeshaji.
11.12 Kazi za Makamu / Katibu wa Bweni.
i)
Atakuwa ndiye kiongozi Mkuu wa eneo la Bweni lake. Kazi zake kusimamia ulinzi na usalama wa Bweni
lake.
ii)
Kupanga na kusimamia kazi za usafi wa eneo lake.
iii)
Kusimamia nidhamu na mwenendo mwema wa wakazi wote wa eneo lake la
Bweni na kutoa Taarifa ya utovu wa
nidhamu wa Mwanachuo yeyote kwa
Mwenyekiti
wa Bweni au kwenye mamlaka ya juu.
iv)
Kuhakikisha kuwa wakazi wote wa eneo lake la ubalozi hawavuti
sigara, hawapiki vyakula, kupiga pasi au kuchemsha maji kwa kutumia ‘heater’ katika
vyumba vya kulala kwa ajili ya usalama wa majengo na Wanachuo wenyewe.
v)
Kutoa taarifa ya wizi au upotevu wa mali ya Chuo au ya Mwanachuo
kwa Mwenyekiti wa bweni au kwa uongozi wa juu.
vi)
Kuhakikisha kuwa daima kuna hali ya utulivu, amani na ushirikiano
mzuri miongoni mwa wakazi wote wa bweni
lake.
11.13 Kamati ya Bweni
i.
Kutakuwa na Kamati ya Bweni katika kila Bweni ambayo itakuwa na
wajumbe wafuatao:-
a)
Mwenyekiti wa Bweni
b)
Katibu wa Bweni (Makamu Mwenyekiti)
ii.
Mwenyekiti wa Bweni ataongoza mikutano yote ya Bweni na Katibu wa
Bweni atakuwa ndiye mwandishi wa vikao vyote vya Bweni.
iii.
Idadi ya wajumbe katika mkutano wa bweni isipungue nusu ya wakazi
wote wa bweni husika.
iv.
Kamati ya bweni itakutana si chini ya mara moja kwa wiki mbili.
11.14 Kamati ya Bweni itakuwa na haki zifuatazo:-
a)
Kusimamia ulinzi na usalama wa bweni ikishirikiana na wajumbe wa
Wizara ya Ulinzi na Usalama.
b)
Kusimamia na kuongoza kazi za kila siku za Bweni kwa maslahi ya
wakazi wa bweni.
c)
Kushughulikia matatizo ya jumla na ya binafsi ya wakazi wa Bweni,
usafi wa bweni wa ndani na nje na kuhakikisha kuwa Bweni linakuwa na utulivu.
d)
Kutekeleza uamuzi wa mkutano wa Bweni na vikao vingine vya juu.
11.15 Wawakilishi wa Madarasa
a)
Kutakuwa na Wawakilishi wawili kwa kila darasa ambao watachaguliwa
na wanachuo wa darasa linalohusika kwa kura za wazi. Viongozi hao watakuwa na
kazi zifuatazo:-
b)
Kusimamia nidhamu ya Darasa lake na kutoa taarifa ya utovu wa
nidhamu wa Mwanachuo yeyote kwa uongozi wa
juu wa ARITASO.
c) Kuweka
kumbukumbu za mahudhurio ya Wanachuo wa darasa kwa kila kipindi na kila siku.
IBARA
YA KUMI NA MBILI
UCHAGUZI NA UTEUZI WA VIONGOZI WA ARITASO
12.1 Tume ya
Uchaguzi.
a) Kutakuwa na
Tume ya Uchaguzi ambayo itasimamia shughuli zote za Uchaguzi wa Viongozi
wa ARITASO chini ya uangalizi na usimamizi wa kamati ya nidhamu.
b) Tume ya
uchaguzi itateuliwa wiki nne baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa masomo.
c)
Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi watachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe wa Tume hiyo.
d) Tume ya
Uchaguzi itakuwa na mamlaka kamili ya
kuendesha na kusimamia chaguzi za
ARITASO kwa mujibu wa taratibu na kanuni za uchaguzi za ARITASO.Tume hii
itakuwa na mamlaka ya kutangaza
matokeo ya chaguzi na ndiyo itakuwa yenye
maamuzi ya mwisho kuhusu masuala ya uchaguzi zaidi ya hapo mwenye kulalamika
juu ya masuala ya uchaguzi atatakiwa akate rufaa.
a)
Waziri wa
Sheria na Katiba atashirikiana na viongozi wa madarasa kupata wajumbe wa Tume ya uchaguzi.
b)
Mwenyekiti
wa Tume ya uchaguzi atawasiliana na mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ili kuiwezesha
Tume hiyo ifanye kazi zake zote kifedha.
c)
Mwenyekiti
wa kamati ya nidhamu atahusika katika mchujo wa wagombea ili kujiridhisha na
mwenendo mzima wa uchaguzi.
d)
Kiongozi
yeyote wa Tume ya uchaguzi ambaye atajihusisha kwenye uchochezi wowote wa
kampeni au rushwa atavuliwa madaraka mara moja na kamati ya nidhamu itakaa mara
moja ili kuchagua mwingine.
e)
Tume
ya Uchaguzi ambayo itajitegemea yenyewe itajumuisha wanachuo wawili kutoka kila darasa na itashughulikia
mambo yote yahusuyo Uchaguzi na taratibu za Uchaguzi.
12.2 Wanachuo wanaostahili kugombea nafasi ya Rais na
Makamu Rais wa ARITASO.
i) Mtu yeyote
aliyesajiliwa kuwa mwanachuo wa Chuo cha Ardhi Tabora anaruhusiwa
kugombea nafasi yoyote
ya uongozi ndani ya Aritaso.Pamoja na hilo atatakiwa kutimiza
vigezo vifuatavyo:
a) Mwanachuo
yeyote anayetarajia kugombea Uongozi katika Serikali ya Wanachuo haruhusiwi
kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
b) Mwanachama
yeyote wa ARITASO ataruhusiwa kuchaguliwa kuwa Rais wa ARITASO ikiwa ana muda
usiopungua mwaka mmoja ndani ya ARITASO.
c) Asiwe kiongozi wa chama chochote
cha siasa Tanzania.
d) Endapo hajatimiza vigezo
na masharti ya kuwa mwanachama wa ARITASO kama
ilivyo tamkwa na katiba hii hataruhusiwa
kugombea nafasi hizo za uongozi.
e) Asiwe ana historia ya
kufanya makosa ya jinai na kuhukumiwa jela kwa makosa hayo
f) Asiwe na histora ya
kufukuzwa au kusimamishwa masomo kwa tuhuma ya utovu
mkubwa wa nidhamu kama vile kujihusisha na ngono, ubakaji,
vurugu dhidi ya
Wanachuo wenzake au wafanyakazi wa Chuo, wizi, Ulevi, uuaji n.k
ii) Chaguzi zingine zote tofauti na Uchaguzi
Mkuu wa ARITASO na uchaguzi wa Spika na
Naibu Spika na Katibu wa Baraza la wawakilishi zinatakiwa kufanyika wiki
moja kabla ya uchaguzi mkuu na zifanyike kwa mujibu wa taratibu na
kanuni za uchaguzi
za ARITASO zitakazo wekwa na Baraza la Wawalikishi.
iii) Viongozi wote wa ARITASO (yaani
Baraza la Uendeshaji, Baraza la Wawakilishi na
Kamati ya Nidhamu) waliopo
madarakani kabla ya kufanyika chaguzi zilizotajwa na katiba hii wataendelea
kubaki madarakani hadi siku ya kuapishwa kwa viongozi wapya. Kwa kiongozi
yeyote atakaye taka kugombea nafasi yoyote ya uongozi atakuwa moja kwa moja
amejiondoa kwenye nafasi yake aliyokuwa nayo kabla hajaamua kugombea nafasi
anayoitaka. Kwa hiyo atahesabiwa kama mwana- ARITASO wa kawaida na si kama
kiongozi tena na nafasi yake atateuliwa mtu mwingine kuishikilia kwa muda kama
kuna ulazima wa kufanya hivyo kama hakuna ulazima itabaki wazi hadi pale
kiongozi mpya atakapo
teuliwa/kuchaguliwa.
iv) Kiongozi yeyote aliyepo madarakani
haruhusiwi kwa namna yoyote ile kuingilia masuala
ya uchaguzi
isipokuwa kamati ya nidhamu pekee au kama kuna jambo la lazima itabidi
awasiliane na Tume ya Uchaguzi.
12.3 Wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa ARITASO
a)
Wanachuo
wote wanaotaka kugombea nafasi ya Urais au Makamu wa Rais watachunguzwa na Tume
ya Uchaguzi baada ya kujaza fomu za maombi.
b)
Mgombea
yeyote atalipia fomu kiasi cha Tsh.10000/= kwenye kamati ya nidhamu na kupewa
stakabaadhi ambayo itamuwezesha kwenda kuchukua fomu ya kugombea kwenye tume ya
uchaguzi.
c)
Muda wa kuchukua na kurudisha fomu hizo
utatangazwa na Tume ya Uchaguzi kwa wanachuo wote. Mgombea atakayejaza fomu
hiyo kabla au baada ya muda uliotangazwa na tume hiyo fomu yake haitajadiliwa
na kwa hiyo jina lake litaondolewa mara moja.
d)
Kama idadi ya wagombea waliochukua fomu
ni zaidi ya wagombea watatu kwenye
kila nafasi
ya uongozi, mchujo utafanyika hadi yabaki majina matatu kwa kila nafasi ya
uongozi.
Mchujo huo utafanywa na Tume ya Uchaguzi baada ya kuwahoji wagombea
kila mmoja
peke yake.
Majina matatu ya wagombea kwa
kila nafasi kati ya nafasi hizo mbili yatafikishwa
kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachuo ili
yapigiwe kura.
e)
Mgombea
atakuwa mshindi kama atapata zaidi ya nusu ya kura zote zitakazopigwa.
Kama idadi ya wagombea waliochukua fomu za
uongozi kwenye nafasi zilizopo ni
chini ya wagombea watatu kwenye kila nafasi
ya uongozi, basi majina yaliyopo ndiyo
yatakayofikishwa kwenye mkutano mkuu wa
wanachuo ili kupigiwa kura. Sio lazima
yawepo majina matatu.
f)
Tume ya Uchaguzi inatakiwa kutangaza
majina ya wagombea waliopitishwa na Tume hiyo kwa ajili ya kupigiwa kura, ndani ya
masaa ishirini na manne baada ya kuwahoji wagombea hao.
g)
Mgombea ambaye jina lake litaondolewa
kwenye kugombea nafasi ya uongozi atapewa barua inayoeleza kwanini ameondolewa kwenye
kinyang’anyiro hicho.
h)
Tume itatakiwa kuendesha chaguzi zote za
viongozi wa ARITASO yaani uchaguzi wa
viongozi wa mabweni, wawakilishi wa madarasa na uchaguzi mkuu ndani ya
siku kumi
toka siku tume hiyo iundwe. Ndani ya siku hizo kumi kutakuwa na siku tatu
za kampeni ambazo zinatakiwa ziwe siku
za masomo ili kuruhusu wagombea kunadi sera zao
Madarasani.Masomo katika siku hizo za kampeni yatasitishwa.
i)
Kutakuwa na karatasi maalum za kupigia
kura ambazo zitaandaliwa na tume ya uchaguzi. Matokeo ya uchaguzi
yatajazwa kwenye fomu maalum zitakazokuwa zimeandaliwa na tume ya uchaguzi na
matokeo ya uchaguzi yatabandikwa kwenye
ubao
wa matangazo.
j)
Endapo mgombea katika nafasi yoyote ya
uongozi hajaridhika na matokeo hayo ataiona tume ili yeye mwenyewe pamoja na
tume wazihesabu kura ili aridhike.
k)
Kama mgombea huyo bado hajaridhika na
matokeo hayo na ana ushahidi wa kutosha juu ya ubadhirifu wa kura, atakata rufaa
kwenye kamati ya nidhamu ya ARITASO kwa
kuandika barua kwa mwenyekiti wa kamati
hiyo ndani ya masaa sita baada ya
matokeo kutangazwa. Mwenyekiti
ataitisha kikao cha kamati ya nidhamu pamoja na tume ya uchaguzi
ili kulijadili suala hilo. Endapo mgombea atashinda kwa kuonyesha ushahidi wa kutosha,
mwenyekiti wa kamati ya nidhamu atatangaza kuwa matokeo ya uchaguzi ni batili
kwa hiyo uchaguzi utarudiwa ndani ya siku mbili tangu kubatilishwa kwa matokeo hayo.Hakutakuwa na kampeni tena na uchaguzi utarudiwa
kwa nafasi iliyoleta utata tu.
l)
Watakaobainika kusababisha
ubadhilifu wa kura watawajibika kwa kuondolewa kwenye tume na watu wengine
watachukua nafasi zao, wala hawatapewa posho ya wajumbe wa tume ya
uchaguzi.
12.4 Uchaguzi wa Spika, Naibu Spika na Katibu wa Baraza la
wawakilishi
i)
Kikao cha kwanza cha Baraza la
wawakilishi kitafanyika ndani ya siku sita baada ya uchaguzi mkuu.
ii) Spika wa Baraza la Wawakilishi atachaguliwa ndani ya siku sita baada
ya uchaguzi mkuu kufanyika
iii)
Endapo
kwa sababu yoyote ile uchaguzi wa Spika utashidikana kufanyika ndani ya siku sita baada ya uchaguzi mkuu, Baraza
la wawakilishi linaweza kuongeza muda wa kufanya uchaguzi huo, muda huo wa
nyongeza usizidi siku tatu na kikao hicho kiwe ni kwa ajili ya kumchagua Spika, Naibu Spika na katibu wa
Baraza la wawakilishi pekee.
12.5 Malipo ya wajumbe wa Tume ya Uchaguzi
Ili kuondoa wasiwasi
Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi hawatalipwa mshahara isipokuwa watawezeshwa kifedha ili
kufanikisha utendaji kazi wao kama ilivyo tamkwa katika ibara ya 10.5 (b) ya katiba hii.
12.6 Mambo
mengine yote yahusuyo utaratibu wa chaguzi za Aritaso yatakuwa kama
itakavyofafanuliwa katika kanuni na taratibu za chaguzi za ARITASO itakayotungwa
na Baraza la wawakilishi.
12.7 Kuapishwa kwa viongozi
Viongozi wafuatayo
watatakiwa kula kiapo cha uaminifu kabla hawaanza majukumu yao katika nafasi
walizo chaguliwa/kuteuliwa.
a)
Rais wa ARITASO, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa ARITASO, hawataanza
majukumu yao waliyopewa ya uongozi mpaka wale kiapo cha uaminifu kwa mkuu wa Chuo,
mbele ya Mshauri wa wanachuo na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya ARITASO.
b)
Spika,Naibu spika na Katibu wa Baraza la wawakilishi hawataanza
majukumu yao waliyopewa mpaka wale kiapo cha uaminifu kwa Mkuu wa Chuo, mbele
ya mshauri wa wanachuo wa Chuo cha ardhi Tabora na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
ya ARITASO.
c)
Mawaziri, Manaibu waziri hawataaza majukumu yao ya uongozi
waliyopewa mpaka wale kiapo cha uaminifu kwa Mkuu wa Chuo mbele ya Mshauri wa
wanachuo wa Chuo cha ardhi Tabora na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya ARITASO.
12.8 Muda wa Kuapishwa.
Rais wa ARITASO atamtangaza Waziri Mkuu na Baraza
la Mawaziri ndani ya siku nne
baada ya uchaguzi mkuu kufanyika kwa ajili ya kuthibitishwa
na Baraza la wawakilishi.
Kwa hiyo viongozi wote wanaotakiwa kula kiapo
cha uaminifu wataapishwa ndani ya siku kumi
baada ya uchaguzi mkuu kufanyika.
IBARA
YA KUMI NA TATU
MAPATO
NA UKAGUZI WA FEDHA ZA ARITASO
13.1 Mapato ya ARITASO yatatokana na:-
a) Miradi
mbalimbali ya ARITASO
b) Zawadi
c) Michango
kutoka kwa Wanachuo na Wafadhili wowote watakaojitokeza.
13.2 ARITASO itaendesha shughuli yoyote itakayokubalika na
mamlaka ya Chuo kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya mfuko wake.
13.3 ARITASO itaweza kuajiri mtu
yeyote kuendesha shughuli za kiuchumi kwa niaba yake ikionekana inafaa kwa
ushirikiano na mamlaka ya Chuo.
13.4ARITASO inaweza kuidhinisha
ukaguzi wa mahesabu (matumizi na mapato) ya fedha kutoka sehemu yoyote ile iwe
ndani au nje ya Chuo.
13.5 Fedha ya ARITASO itakaa
kwenye account ya ARITASO.
13.6 Fedha ya ARITASO itatumika
kwa manufaa ya ARITASO tu kadri yatavyopangiliwa na Baraza la Wawakilishi
pamoja na Baraza la Uendeshaji la ARITASO.
13.7 Waziri wa fedha au
Katibu wa Wizara hiyo ndio watakaofuatilia michango kutoka kwa
mhasibu wa Chuo na kuzipeleka Benki
13.8 Wizara ya fedha itabuni miradi
ili fungu la Wana ARITASO liongezeke.
13.9 Waziri wa fedha ataandaa
taarifa ya fedha ya kila mwezi na ataisambaza kwenye mihimili yote mitatu ya ARITASO si chini ya
mara mbili kila muhula wa masomo.
13.10 Kutakuwa na taarifa ya
mkaguzi wa ndani wa mahesabu ya akaunti zote za Chuo cha Ardhi Tabora kila mwaka .
13.11
Rais wa ARITASO
ataidhinisha malipo yote ya ARITASO.
13.12
Waziri wa fedha atamkabidhi
waziri mkuu vivuli vya Nyaraka zote za mapato na matumizi ya ARITASO kila baada
ya siku kumi na nne.
13.13 Fedha zote za ARITASO
zirejeshwe benki kabla ya kwenda likizo au mafunzo kwa vitendo. Kwa waziri
yeyote atakaye ondoka na fedha za ARITASO bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa
katibu Mkuu wa ARITASO Mwenyekiti wa ARITASO atakuwa na uwezo wa kumpa barua ya onyo kali na ikiwezekana
kuvuliwa madaraka aliyonayo.
IBARA YA KUMI NA NNE
MENGINEYO:
14.1Mambo ya Kuzingtia
i)
Orodha ya majina na picha za viongozi wa ARITASO itaifadhiwa
katika
nyaraka za ARITASO
ii)
Hakuna Mwanachuo au kikundi cha Wanachuo kitakachotumia jina la
ARITASO bila idhini ya maandishi ya
Katibu Mkuu wa ARITASO.
iii)
Mshauri wa wanachuo ( Dean
of student) ndiye atakayekuwa mshauri mkuu wa serikali yote ya ARITASO na
atatakiwa kuhudhuria vikao vyote vya wanachuo wa chuo cha Ardhi Tabora.
iv)
Kila kiongozi atapewa cheti cha uongozi
katika nafasi aliyokuwa nayo.Vyeti
hivi vitaadaliwa
na uongozi utakaoingia madarakani na ili kiongozi apewe cheti, lazima atimize kipengele cha (14.1.9) cha
katiba hii na lazima aidhinishwe na
Baraza la uendeshaji la uongozi
mpya kwa kushirikiana na mshauri wa wanachuo
v)
Mwanachuo wa Chuo cha Ardhi Tabora akifiwa na Baba, Mama, Mke,
Mume au Mtoto atapatiwa pole kiasi cha shilingi Elfu 40,000/= kutoka kwenye
mfuko wa ARITASO.
vi)
Mwana ARITASO wa kike akipata mimba aruhusiwe kuahirisha masomo na
baadaye kurudia mwaka alioachia kwa ruhusa ya Bodi ya Chuo pasipo kipingamizi
chochote.
vii)
Kutakuwa na Wawakilishi
watatu (Waziri wa Elimu, Naibu Waziri wa Elimu na mjumbe mmoja wa Wizara) wa
ARITASO kwenye kamati ya mitihani ya Chuo itakayotathimini matokeo ya mitihani
ya mwisho wa mwaka.
viii)
Kutakuwa na Wawakilishi wa ARITASO kwenye kamati ya chakula ya
Chuo itakayoshughulikia masuala ya chakula cha Wanachuo itakayoamua hatua ya
chakula kisichoridhisha.
ix)
Kiongozi ambaye hakumaliza muda wake wa
uongozi kwa sababu mbalimbali
mfano kujiuzuru, kuondolewa
kwenye uongozi kwa sababu ya ubadhilifu wa
mali ya umma au uzembe au utovu wa
nidhamu,hatapewa cheti cha uongozi.
Ili kiongozi apewe cheti ni lazima awe amekaa
madarakani kwa muda
usiopungua angalau miezi mitatu.
x)
Marufuku
kwa waziri yeyote kwenda likizo na nyaraka za
ARITASO. Kila kiongozi azirejeshe nyaraka za sekta yake kwenye ofisi
ya
ARITASO
kabla ya kuondoka kwenda likizo.
x i)
ARITASO kwa kushirikiana na mshauri wa
wanachuo itatakiwa kuandaa ripoti ya
kila mwisho wa mwaka na kuipeleka kwenye uongozi wa chuo.
x ii) Kiongozi
yeyote wa ARITASO asiyewajibika kwenye nafasi yake ya uongozi bila taarifa
yoyote kwa uongozi wa ARITASO hatahusika katika mchakato wa kuwezeshwa kifedha.
IBARA YA KUMI NA TANO
MAREKEBISHO YA KATIBA
i)
Katiba hii inaweza kufanyiwa marekebisho endapo theruthi mbili ya
wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi
watakubali uamuzi huo. Kinachotakiwa Waziri wa sheria na katiba ataandaa
muswada wa marekebisho ya katiba kwa kuzingatia sheria na taratibu za chuo.
ii)
Baraza la wawakilishi litaunda kamati maalum ya marekebisho ya
katiba ambayo itakusanya maoni juu ya
muswada uliotolewa wa marekebisho ya katiba.
iii)
Kamati ya baraza la wawalikishi ya kushughulikia marekebisho ya
katiba,itakusanya na kuyawasilisha
kwenye baraza la wawakilishi maoni na mapendekezo juu ya marekebisho ya katiba
hii kwa ajiri ya kutolewa maamuzi.
iv)
Baraza la wawakilishi litayatolea maamuzi maoni na mapendekezo ya
marekebisho ya katiba kwa kusahihisha, kupunguza au kuongeza maoni au
mapendekezo mengine kadri litakavyoona inafaa.
v)
Ili kurekebisha katiba hii baraza la wawakilishi litaitisha kikao
maalum kwa ajili ya marekebisho ya katiba na theluthi mbili ya wajumbe wote wa
baraza la wawakilishi wanatikiwa kuhudhuria.ili kupitisha maamuzi ya kurekebisha
katiba hii theruthi mbili ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho wanatakiwa
kukubali uamuzi huo.
vi)
Rasimu ya katiba itaandaliwa na kuwasilishwa kwa wanachuo ili
kutolewa maoni ikikubaliwa inatangazwa rasmi na mkuu wa chuo kuwa katiba ya ARITASO.